Umoja wa Viongozi wa madhehebu ya dini nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati wameonesha imani kubwa ya ulinzi wa amani unaotolewa na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania nchini humu.
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti mara baada ya kutembelewa na Kamanda wa Kikosi cha Nane cha
Ulinzi wa Amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati Luteni Kanali Theofili Nguruwe
wamesema uwepo wa JWTZ umekuwa na tija sana nchini humo kwani wamekuwa
wakifanya kazi zao kwa weledi wa hali ya juu.
Akizungumza
kwa niaba ya Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Berberati Mhashamu
Koffi Denis, Karibu Mkuu wa Jimbo hilo Padre Jean Ancelimo amesema mbali na
Ulinzi wa Amani pia limekuwa likitoa misaada mbalimbali ya hali na mali huku
akitolea mfano wa ujenzi wa shule ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
(TEHAMA) ambayo imepewa jina la Serengeti.
Naye
Askofu Mkuu wa Kanisa la Evenjeliko (AEC) Mhashamu Lucian Nday amesema uwepo wa
JWTZ nchini hapo umewafanya waishi kwa amani na zaidi ya yote limewezesha
ukuaji wa lugha adhimu ya kiswahili.
Sheikh
Rashid Mohamoud Arouna ni Imam wa Masjid Nuur amesema JWTZ limekuwa mstari wa
mbele kwenye kila jambo ambalo wanaombwa kutoa msaada kwa ajili ya kuhakikisha
nchi yao inakuwa na amani.
Kwa
upande wa Kamanda wa Kikosi cha Nane cha Ulinzi wa Amani nchini Jamhuri ya
Afrika ya Kati Luteni Kanali Theofili Nguruwe amewashukuru viongozi hao na
kuahidi kutekeleza majukumu yake kwa weledi wa hali ya juu.
0 Maoni