Mamlaka
ya Mapato Tanzania (TRA) inatarajia kushirikiana na Baraza Kuu la Waislamu
Tanzania (BAKWATA) kutoa Elimu ya Kodi ili kuhamasisha Wananchi kulipa kodi kwa
hiari.
Hayo
yamebainishwa wakati wa mazungumzo baina ya Kamishna Mkuu wa TRA Bw. Yusuph
Juma Mwenda alipomtembelea na kufanya mazungumzo na Mufti na Sheikh Mkuu wa
Tanzania Dr. Sheikh Abubakar Ali Zubeir kwenye Ofisi za BAKWATA Jijini Dar es
Salaam.
Wakati
wa mazungumzo yao Kamishna Mkuu Mwenda amesema licha ya kwenda kumtakia Heri ya
Mwaka Mpya Mufti pia ameenda kuomba ushirikiano katika eneo la Elimu kwa
Mlipakodi ili kuwezesha kuongeza uelewa zaidi wa masuala ya Kodi kwa jamii.
Amesema
kuwa TRA itatoa Elimu ya Kodi kwa Viongozi wa Dini zote kwa Nchi nzima ili
pawepo na uelewa wa pamoja utakaosaidia Viongozi hao kufikisha elimu hiyo kwa
waumini wao.
"Suala
la Kodi ni la kiibada hivyo kuhamasisha Kodi ni kuhamasisha Ibada jambo ambalo
ni jema na linasaidia katika maendeleo ya nchi," amesema Kamish.
0 Maoni