Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) leo Jumanne
Januari 14, 2025 imetoa taarifa ya uwepo wa Kimbunga Dikeledi katika Bahari ya
Hindi mwambao wa pwani ya Msumbiji.
Taarifa ya mamlaka hiyo imeeleza kuwa mifumo ya hali ya
hewa inaonesha kimbunga hicho kwa sasa kipo mwambao wa pwani ya Msumbiji na
kinatarajiwa kurejea katika Rasi ya Msumbiji leo alasiri huku ikibainisha kuwa
kimbunga hicho hakiashirii uwezekano wa kusababisha athari za moja kwa moja
hapa nchini.
Hata hivyo, kutokana na ukaribu wa maeneo ambayo Kimbunga
Dikeledi kipo sambamba na maeneo ya kusini mwa nchi yetu, upo uwezekano mdogo
wa matukio ya vipindi vifupi vya mvua kubwa katika maeneo ya pwani ya kusini
hususan katika mikoa ya Lindi na Mtwara kwa siku ya leo Januari 14, 2025, imeeleza
taarifa hiyo.
0 Maoni