Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), limewapongeza viongozi
wa Chama cha Mapinduzi (CCM) waliochagulia na kuteuliwa katika nyadhifa
mbalimbali.
Hapo jana katika Mkutano wake Mkuu Maalum CCM walimteua Rais
Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea wa urais 2025 na Dkt. Balozi Emmanuel
Nchimbi kuwa mgombea wake mwenza.
Aidha, Dk Hossein Ali Mwinyi ameteuliwa kuwa mgombea wa urais kwa upande wa Zanzibar. Pia kada mkongwe Stephen Wassira akichagulia kuwa Makamu wa Mwenyekiti wa chama hicho Bara.


0 Maoni