Mtu mmoja ambaye alikuwa akigua ugonjwa wa Marburg
amegunduliwa nchini Tanzania.
Akizungumza katika mkutano na Katibu Mkuu wa Shirika la
Afya Duniani WHO Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan
amesema kwamba serikiali yake ilichukua hatua kufuatia uvumi uliokuwa
ukiendelea katika eneo la Kagera.
Amesema kwamba sampuli zilizochukuliwa katika hospitali
moja mjini Kagera na kuthibitishwa mjini Dar es Salaam zilimtambua mtu huyo
aliyekuwa na virusi vya maradhi hayo.
Hatahivyo sampuli za washukiwa wengine wa maradhi hayo
hazikupatikana na ugonjwa huo hatari.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa WHO Dkt. Tedros Adhanom
Ghebreyesus amesema wamedoa dola za Marekani milioni 3 ili kusaidia Tanzania kudhibiti
maradhi hayo, ikiwa ni pamoja na dola 50,000 ambazo shirika hilo lilitoa ili kusaidia
katika uchunguzi.
Dkt. Adhanom
amesema kufikia sasa hakuna chanjo wala tiba iliothibitishwa kukabiliana na
virusi vya Marburg licha ya kwamba kuna mipango ya kuafikia hayo.
Dkt. Adhanom ameongezea
kuwa milipuko inaweza kudhibtiwa kupitia mikakati ya kuzuia maambukizi na
kuokoa maisha kama ilivyofanya Tanzania.

0 Maoni