Maelfu ya raia wameripotiwa kukimbia mapigano kati ya
jeshi la nchi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na waasi wa kundi la M23
mashariki mwa nchi hiyo.
Jeshi na washirika wake wamekuwa wakipambana kuukomboa
mji wa Masisi ambao hivi karibuni uliangukia mikononi mwa waasi hao.
Mashirika ya misaada ya kibinadamu yameonya kuwa raia
wako katika hatari kubwa huku silaha nzito zikitumiwa katika maeneo ya makazi ya
raia vitongojini.
Waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda wanaonekana
kudhamiria kupanua sehemu wanayodhibiti katika eneo mashariki mwa Kongo lenye
utajiri wa madini.

0 Maoni