Rais Trump atia saini amri ya Marekani kujitoa WHO

Rais wa Marekani Donald Trump ametia saini amri ya ya kuanza mchakato wa kuiondoa Marekani kuwa mwanachama wa Shirika la Afya Duniani (WHO).

Rais huyo mpya wa Marekani alisema “Hili ni jambo kubwa” wakati alipokuwa akiidhinisha hati hiyo baada ya kurejea tena katika Ikulu ya Marekani.

Amri hiyo ni moja ya amri kadhaa za utendaji alizotia saini rais Trump katika siku ya kwanza tu aliyoingia madarakani.

Hii ni mara ya pili kwa Trump kuamuru Marekani kujiondoa kuwa mwanachama wa WHO.

Rais Trump pia ametia saini agizo la kuipa TikTok nyongeza ya siku 75 ili kutii sheria inayotaka iuzwe au kupigwa marufuku nchini Marekani.


Chapisha Maoni

0 Maoni