Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi
amewahakikishia Wananchi kuwa Serikali
inatenga kiasi cha Dola za kimarekani Millioni 10 sawa na Shillingi
Billioni 300 kwa mwaka kwa ajili ya
kulipa madeni ya Nchi.
Rais
Dk. Mwinyi ameeleza kuwa wakati Serikali inakopa kwa ajili ya Miradi ya
Maendeleo Ina Akaunti Maalum
inayoweka Fedha za kutosha Kulipa Madeni hayo ambayo sasa ina kiasi cha
Shillingi Biliioni Mia Sita.
Rais
Dk. Mwinyi ameyasema hayo alipofungua Kituo cha Mabasi Kijangwani Wilaya ya
Mjini,Mkoa wa Mjini Magharibi kilichojengwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (ZSSF).
Amefahamisha
kuwa deni ililonalo Zanzibar kwa sasa ni Shillingi
Trilion 1.2 linaloaminika na kuwa
na uwezo wa kukopesheka tena
kutokana na utaratibu huo uliopo Serikali inaweza kulilipa kipindi cha
miaka miwili.
Aidha,
ameeleza kuwa Wakati Serikali ya Awamu ya Nane inaingia Madarakani deni la
Serikali lilikuwa Shillingi Bilioni Mia nane na sasa baada ya miaka minne
limepanda hadi kufikia Trilioni 1.2
Rais
Dk. Mwinyi amekanusha vikali taarifa zilizotolewa na Wapinzani hivi karibuni
kuwa Zanzibar ina deni linalofikia Trilioni 2.8 sawa na ongezeko la asilimia
208 kuwa za Uongo na Propaganda za Kisiasa zisizo sahihi.
Amesisitiza
kuwa Serikali inakopa kwa nia njema ya Kuendesha Miradi ya Maendeleo yenye tija
na maslahi kwa nchi na sio vyenginevyo.
Akizungumzia
kituo hicho kipya cha Mabasi ameutaka Mfuko wa Hifadhi ya Jamii ZSSF kuwa
na Mpango maalum wa Matunzo na
Usafi na
kuandaa ajira Maalum kwa Vijana kwa ajili kutoa huduma hizo.
Halikadhalika,
Rais Dk.Mwinyi amefahamisha kuwa Serikali inakuja na Mpango Mkuu wa
Usafiri utakaoifanya nchi kuwa na
Usafiri wa Kisasa na Huduma Bora.
Mpango
huo utajumuisha Ujenzi wa Vituo vya Kisasa vya Mabasi katika Maeneo ya Chuini,
Jumbi , Mwera na Mwanakwerekwe pamoja na Kijangwani ,Malindi na Mnazi Mmoja kwa
Eneo la Mjini kusisitiza kuwa kabla Mwisho wa Mwaka huu Zanzibar itaanza kutumia Mabasi Ya Umeme.
0 Maoni