Nyangumi aliyevutia dunia mwaka 2018, alipoonekana akisukuma mwili wa mtoto wake aliyekufa kwa siku 17, ameonekana tena akiomboleza baada ya kupoteza mtoto.
Nyangumi
huyo anayejulikana kama Tahlequah, amepoteza mtoto na safari hii pia anausukuma
mwili wa mtoto wake huyo, Kituo cha tafiti za nyangumi kimesema.
Nyangumi
Tahlequah ameonekana kando ya pwani ya jimbo la Washington nchini Marekani.
Nyangumi
wa aina hiyo wanafahamika kwa tabia ya kusukuma miili ya watoto wao
wakiomboleza kwa muda wa wiki, lakini wanasayansi wamesema Tahlequah ameweka
rekodi.
0 Maoni