Mbunge
wa Jimbo la Mafinga na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki Mhe. Cosato Chumi (Mb) ametembelea TFS-Shamba la Miti Sao Hill ili
kuona namna shughuli za upandaji miti na uhifadhi wa misitu zinazofanywa na
Shamba leo Januari 03, 2025.
Waziri
Chumi ameipongeza TFS kupitia Shamba la Miti Sao Hill kwani imekuwa na mchango
mkubwa kiuchumi kwa wakazi wanaolizunguka shamba kwani limekuwa likichangia
uendelezaji wa miradi mingi ya maendeleo hususani katika Wilaya ya Mufindi na
Taifa kwa ujumla.
Aidha
amesema kuwa Shamba la Miti Sao Hill limekuwa msingi mkubwa wa uzalishaji wa
malighafi za viwanda hali iliyochangia kukua na kuongezeka kwa uwekezaji wa
viwanda vya mazao ya misitu katika Wilaya ya Mufindi.
Pamoja
na hayo amewataka wahifadhi kuendelea kutoa elimu ya uhifadhi kwa wananchi
wanaolizunguka shamba ili kuendeleza uhusiano mzuri iliopo baina ya Shamba na
wananchi pamoja na kuongeza jitihada za
ulinzi wa rasilimali misitu dhidi ya majanga ya moto yanayoweza kujitokeza na
ambayo yamekuwa yakijitokeza mara kwa mara na kuharibu rasilimali hiyo.
Ameongeza
kuwa ni wakati sasa kwa viongozi wa ngazi zote Wilayani Mufindi kushirikiana
kwa pamoja ili kuhakikisha shughuli za uhifadhi zinafanyika kwa ufasaha na
kuhakikisha elimu ya uhifadhi inawafikia wananchi wote.
0 Maoni