Jeshi
la Polisi Mkoa wa Mbeya kwa kushirikiana na maafisa wa Shirika la Umeme nchini [TANESCO]
linawashikilia watuhumiwa wawili Movin Joseph Mwaholi [53] Mfanyabiashara wa
vifaa vya umeme na Rehema Jamson Silia [42] Mfanyabiashara wa chuma chakavu,
mkazi wa nzovwe kwa tuhuma za kukutwa na miundombinu ya umeme na maji.
Watuhumiwa
walikamatwa Januari 02, 2025 katika oparesheni ya pamoja iliyofanywa na Jeshi
la Polisi kwa kushirikiana na maafisa wa shirika la umeme [TANESCO] kanda ya
nyanda za juu kusini katika eneo la uwanja wa ndege wa zamani mtaa wa Block T
Jijini Mbeya katika godown la mfanyabiashara Movin Joseph Mwaholi.
Taarifa
ya polisi Mbeya imesema watuhumiwa walikutwa na vifaa mbalimbali vya umeme na
maji ikiwemo harking hons 57pcs, spindle 128 pcs, inlate cape 35 pcs, gaskate
cover, bolt, nuts, copper wire, aluminium wires, bib tape ¾ 43 pcs, gate valve
¾ 35 pcs, black nut ¾ 5 pcs, mfuniko wa mita 1 pc. Baadhi ya vifaa hivyo ni
vile vilivyofunguliwa kwenye miundombinu ya umeme, Transformer na miundombinu
yamaji ambayo imetambuliwa na maafisa wa TANESCO na Mamlaka yamaji safi na
usafi wa mazingira Mbeya.
Jeshi
la Polisi Mkoa wa Mbeya linaendelea kutoa wito kwa baadhi ya wananchi wenye
tabia ya kuhujumu miundombinu ya nchi ikiwemo ya Umeme na Maji kuacha mara moja
kwani uhalifu hauna nafasi wala haulipi ni vyema wakafanya shughuli nyingine
halali. Vitendo hivyo wanavyofanya vinarudisha nyuma juhudi za Serikali ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hivyo Jeshi la Polisi litaendelea na
oparesheni hii na wale wote watakaobainika watachukuliwa hatua kali kwa mujibu
wa sheria ikiwepo kufikishwa mahakamani.
0 Maoni