Rais Samia adhamiria wananchi kupata matibabu ya uhakika - Balozi Kombo

 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo amesema, dhamira njema ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuipa kipaumbele Sekta ya Afya nchini ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma za uhakika za matibabu bila kuzifuata nje ya nchi.

"Vission yake ni kwamba wasitoke wagonjwa kutoka Zanzibar kwenda kutibiwa nje ya nchi. Watatibiwa hapa hapa, huo ndiyo muono wake;

Ameyasema hayo katika hafla ya ufunguzi wa Kituo cha Afya Kizimkazi Wilaya ya Kusini Unguja ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.

"Mbali ya kutoa neno moja kutoka Muungano, naomba nichukue fursa hii, Mheshimiwa kukujulisha kwamba mimi nilishirikishwa katika initiative hii ya Samia Foundation.”

"Na ninaomba niwaambie wananchi na hasa kwa Wizara ya Afya kupitia Mheshimiwa Nassor Mazurui ambaye naye anaifahamu vission ya Mama Samia kwa Zanzibar na Sekta ya Afya na hapa Kizimkazi.

"Katika vission hiyo, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Kikwete tulitumwa pia kwenda kuangalia pale Jakaya Kikwete Cardiac Institute kuangalia mifumo yao.

"Kwa hiyo naomba niseme hii ni asilimia ndogo sana ya Mama Samia Foundation na hiki Kituo cha Kizimkazi, muundo wake na vission yake ninaweza kusema ni kubwa zaidi.

"Ninaweza kusema ni chini ya asilimia ya asilimia 10 sasa hivi, lakini muundo na vission yake ni kubwa zaidi."

Pia, amempongeza Mhandisi...kwa kuteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Samia Foundation.

Amesema, uteuzi wake utamsaidia Rais Dkt. Samia kutafsri ndoto yake pana kama alivyoweza kufanya Dkt.Jakaya Kikwete na leo wagonjwa wengi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wanapata huduma zao Dar es Salaam bila kwenda nje ya nchi.

Pia, amempongeza Rais Dkt.Samia kwa kuweka msukumo mkubwa katika upatikanaji wa nishati ya uhakika, hatua ambayo imeungwa mkono na viongozi wengi ndani na nje ya Afrika.




Chapisha Maoni

0 Maoni