Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa akizungumza na askari wa usalama
barabara katika eneo la Magugu wilayani Babati mkoani Manyara wakati akiwa
safari mara baada ya kushudia askari hao wakitekeleza majukumu yao kwa weledi
na uadilifu, leo tarehe 04 Januari 2024.
Bashungwa
akiwa kwenye gari lenye namba za usajili binafsi, direva wake alisimamishwa na
kuanza kukaguliwa wakati Waziri huyo akiwa ndani ya gari ambapo baada ya
kuruhusiwa, aliwaita askari hapo na kuwapongeza kwa kutekeleza majukumu yao kwa
weledi.
“Nimeshamwambia
IGP, barabarani sio machinjio ya watu, kwahiyo mnaposimamia majukumu yenu kwa
weledi tunafurahi. Hakuna ambaye yupo juu ya sheria, mtu yeyote anayetumia
chombo cha moto anapokuwa barabarani lazima azingatie sheria za usalama
barabarani,” Bashungwa akizungumza na askari.
Aidha,
Bashungwa amempongeza Kamishna Mwandamizi wa Jeshi la Polisi (SACP) William
Mkonda, Mkuu wa Kikosi cha Usalama barabarani, Maafisa na Askari wote wa
Usalama Barabarani na kuwataka kuendelea kushughulika na madereva wazembe.
“Mwaka
2025 tushushe sana takwimu za vifo vya ajali barabarani kama ambavyo mhe. Rais
Dkt. Samia Suluhu Hassan alivyosikitishwa kwenye hotuba ya kufunga mwaka 2024
na kukaribisha mwaka 2025 na kuagiza Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na Jeshi
la Polisi kutafuta suluhu ya ajali nyingi barabarani.”
0 Maoni