Mwanamke
raia wa Japani, anayetambuliwa kama mtu mzee zaidi duniani na Guinness World
Records, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 116.
Mwanamke
huyo Tomiko Itooka amefariki katika makazi ya wazee katika jiji la Ashiya, Mkoa
wa Hyogo, kulingana na maafisa.
Itooka
alikuwa mtu mzee zaidi ulimwenguni baada ya Maria Branyas Morera wa Uhispania
kufariki mnamo Agosti 2024 akiwa na umri wa miaka 117.
"Bi
Itooka alitupa ujasiri na matumaini kupitia maisha yake marefu,"Meya wa
Ashiya mwenye umri wa miaka 27 Ryosuke Takashima amesema katika taarifa.
Bi
Itooka alizaliwa Mei 1908 - miaka sita kabla ya Vita vya Kwanza vya Dunia na
mwaka huo huo ambao gari la Ford Model T lilizinduliwa nchini Marekani.
0 Maoni