Wakizungumza
wakati wa ziara ya waandishi wa habari kutembelea miradi ya ujenzi wa
miundombinu wilayani humo wakazi hao wamesema kabla ya ujenzi wa miundombinu
hiyo walikuwa wakipata shida hasa kipindi cha mvua zilizokuwa zikisababisha
mafuriko na kukata mawasiliano kutokana na kutokuwa na madaraja ya kutosha
wilayani humo.
Bi.
Angelina Makala mkazi wa Kijiji cha Lolotu wilayani humo anasema kipindi cha
nyuma kabla ya ujenzi wa miundombinu hiyo walikuwa wanashindwa kwenda kwenye
shughuli zao za kijamii kutokana na maji kujaa katika mito na kukatisha
mawasiliano.
“Kipindi
cha nyuma tulikuwa tunateseka, maana kipindi cha masika tunavuka maji
tunaogelea kwenye maji na shule watoto hawaendi mpaka mafuriko yaishe. Lakini
tangu hii barabara imejengwa huu ni mwaka wa tatu tunanufaika na hii barabara.
“Tunashukuru
kwa sababu hata juzi hapa maji yalitoka, tumeona ni vema Mama Samia anatufanyia
vizuri, mkandarasi aliyeshika hapa anajenga makalavati makubwa,” alisema
Angelina.
Naye,
Bw. Cloud Losioki mkazi wa Orkesumet, wilayani Simanjiro anasema kwa mara ya
kwanza mji wao umepata Barabara za lami ambazo zimesaidia kurahisisha usafiri
pamoja na kuwaepusha na athari za kiafya ambazo awali zilikuwa zikisababishwa
na vumbi kutokana na barabara kutokuwa na lami hivyo kuishukuru serikali kwa
kuwapelekea mradi huo.
Amesema
kukamilika mradi huo kutawasaidia kuwainua kiuchumi kutokana na maendeleo
yatakayopatikana ikiwemo kusafirisha mazao na bidhaa nyingine kwa urahisi kwa
kutumia barabara hizo.
“Tunafurahi
kwa sababu ni kwa mara ya kwanza kabisa ndani ya mji wetu huu tunapata barabara
ya lami, naamini kabisa kwamba kila mtu anafurahia sababu barabara ya lami
inasaidia kupunguza vumbi, wakati mwingine tunakuwa na migahawa pembeni, kama
barabara ni za vumbi, vumbi yote zinaingia kwenye chakula wateja wanaathirika
kutokana na vumbi na vitu kama hivyo, unapopata barabara za lami mojawapo ya
athari za kiafya zinapungua, lakini pia barabara za lami tunazopata
zinarahisisha sana usafiri, alisema Cloud.
Alisema
kikamilika kwa barabara hizo mji wa Orkesumet utapendeza na kukua kiuchumi
ambapo hata hivyo aliomba serikali kuwawekea lami katika barabara kuu ya kutoka
Arusha na kuunganisha wilaya ya Kiteto ili kuleta maendeleo kwa wananchi wa mji
huo.
Awali
akizungumza na waandishi wa habari Kaimu Meneja wa Tarura Wilaya ya Simanjiro,
Mhandisi Naftari Chaula amesema kazi yao kubwa ni kuhakikisha wanasimamia
mtandao wa barabara pamoja na matengenezo na kwamba katika wilaya hiyo
wanasimamia barabara yenye urefu wa Kilometa 1368.
Amesema
Barabara ya kiwango cha changarawe ni Kilometa 230, Kiwango cha udongo zaidi ya
Kilometa 1,000 na Kilometa 4.5 ni kiwango cha lami ambapo lengo ni kufikia
Kilometa 6.5 mpaka kufikia mwezi Februari mwaka huu.
Aidha,
Mhandisi Chaula amesema kumekuwa na mabadiliko makubwa ya Bajeti ya utekelezaji
wa matengenzo ya barabara ambapo utoaji wa fedha umeongezeka kutoka Shilingi
Milioni 960/- hadi kufikia Bilioni 4.5/-.
Hata
hivyo amesema wanategemea kufungua barabara zaidi ya Kilometa 140 katika eneo
la Kitwai kwa ajili ya kuanzisha makazi mapya katika eneo hilo ambapo serikali
imetenga fedha kwa ajili ya mradi huo.
Kwa
upande wa Mji wa Mererani, Mhandisi Chaula amesema mwaka jana wamejenga
barabara ya lami yenye urefu wa Kilometa 1.22 na kuweka taa 31 na kufanya
mabadiliko makubwa katika Mji wa Orkesumet kwa kuweka lami Kilometa 1.9.
Kujengwa
kwa barabara hizo katika meneo hayo kutasaidia kuongeza thamani ya ardhi lakini
pia kuchochea ukuaji wa shughuli za kila siku pamoja na kuboresha mazingira
safi yatakayopelekea kuimarika kwa afya bora za wananchi.
0 Maoni