Rais wa Kenya William Ruto anatarajiwa kusafiri leo Jumatatu Januari 6, 2025 kwenda Accra Ghana kuhudhuria sherehe ya kuapishwa rais mteule John Dramanu Mahama Januari 7, 2025.
Rais
Ruto pia anatarajia kutumia sherehe hizo kukutana na marais wengine wa Afrika
kwa ajili ya kumpigia debe Raila Odinga ambaye anawania Uenyekiti wa Tume ya
Umoja wa Afrika.
Wiki
iliyopita Rais Ruto alimualika Kenya Rais Mahama nyumbani kwake Kiligoris huko
Narok, katika jitihada za kumpigia kampeni Raila Odinga kufanikiwa kutwaa
nafasi hiyo ya AU.
0 Maoni