Mwandishi
wa Habari wa AYO TV Eugene Peter anatafutwa na familia yake pamoja na ofisi
yake ya Dar es Salaam baada ya kutoweka
bila kujulikana alipo leo ikiwa ni siku ya tisa.
Mara
ya mwisho Eugene alionekana mazingira ya nyumbani kwake Jumapili Desemba
29,2024 majira ya saa mbili usiku.
Familia
akiwemo Baba yake mzazi na watu wa karibu wamethibitisha kutokuwa na mawasiliano
naye tangu wakati huo ambapo Dar es Saalam hajaonekana na kwao Arusha na Moshi
hajafika huku simu zake zikiwa hazipatikani.
Baada
ya jitihada kubwa za kumtafuta maeneo mbalimbali na kutoa taarifa ya kupotea
kwake Polisi, AyoTV na Familia kwa pamoja tunaomba mtu mwenye taarifa kumuhusu
apige simu namba 0769401050 au aripoti kituo cha Polisi kilicho karibu nae.
0 Maoni