Jeshi
la Polisi limetangaza kupokea taarifa ya kupatikana kwa Mtangazaji wa TV 3,
Gwamaka Francis Gehas Mkazi wa Mbezi Beach Africana ambaye aliripotiwa na na
chombo hicho cha habari kuwa alipotea mnamo Januari 03, 2025 majira ya mchana.
Taarifa
ya Msemaji wa Jeshi la Polisi, Makao Makuu ya Polisi Dodoma imebainisha kuwa
baada ya ufuatiliaji ulioanza kwa kukusanya ushahidi na taarifa kutoka kwa watu
mbalimbali na leo Januari 5, 2025 majira ya saa kumi na moja jioni Jeshi la
Polisi limepokea taarifa kuwa amepatikana na yupo Kitunda nyumbani kwa shangazi
yake.
Aidha,
Jeshi la Polisi limesema linaendelea na uchunguzi ikiwa ni pamoja na kupata
maelezo yake ili kupata uhalisia wa tukio la kutokuonekana kwake na baadaye
kuonekana akiwa kwa shangazi yake.
“Uchunguzi
huu utatusaidia kupata ukweli kuna kitu gani nyuma yake ili hatua stahiki
zichukuliwe kulingana na ushahidi utakaopatikana,” imemalizia kusema taarifa
hiyo ya polisi.
0 Maoni