Mamilioni
ya watu wakumbwa na baridi kali huku majimbo sita ya Marekani yakitangaza hali
ya dharura.
Mamilioni
ya Wamarekani wamearifiwa kujiandaa kwa hali ya hewa ya majira ya baridi. Jimbo
la West Virginia limeungana na majimbo mengine matano kutangaza hali ya
dharura.
Kentucky,
Virginia, Kansas, Arkansas na Missouri zimetangaza hali ya dharura.
Majimbo
30 ya Marekani yanayoanzia katikati mwa nchi hadi pwani ya mashariki - ikiwa ni
pamoja na miji mikuu kama Washington DC na Philadelphia, yanatarajiwa kushuhudia
baridi kali.
Watabiri
wa hali ya hewa wanasema mgandamizo mkubwa wa hewa kutoka katika nguzo mbili za
dunia umeleta baridi kutoka Aktiki hadi katikati ya Marekani na kusababisha
hali mbaya ya hewa.
0 Maoni