Rais Mwinyi kula chakula cha mchana na Zanzibar Heroes

 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Dkt. Hussein Mwinyi ameialika timu ya  Taifa ya Zanzibar, Zanzibar Heroes Ikulu kwa chakula cha mchana siku ya Jumatano  tarehe 15 Januari 2025.

Rais Dk. Mwinyi ametoa mwaliko huo Uwanja wa Gombani Pemba baada ya timu hiyo kufanikiwa kulitwaa Kombe la Michuano ya Mapinduzi  2025.

Zanzibar Heroes  imeifunga timu ya Taifa ya Burkinafaso  kwa magoli 2-1 katika mchezo mkali wa fainali uliochezwa uwanja wa Gombani  Mgeni Rasmi akiwa Rais Dk. Mwinyi ambae  alikabidhi kombe kwa bingwa wa michuano hiyo Zanzibar Heroes.

Zanzibar Heroes ilitinga fainali badaa ya kuilaza timu ya taifa ya Kenya Harambe Stars kwa goli 1-0. Licha ya kombe la ubingwa timu hiyo pia imejinyakulia kitita cha Shilingi Milioni 100.




Chapisha Maoni

0 Maoni