Polisi mkoani Pwani wamefanikiwa kumpata mtoto mwenye
umri wa miezi sita aliyechukuliwa na watu wasiojulikana, baada ya kuvamia
nyumba ya Melksedek Mrema na mkewe Joan Gabriel, ambao nao wakati wa tukio hilo
walitupwa kwenye mashimo ya choo, kabla ya watuhumiwa kuondoka na mtoto huyo
pamoja na gari.
Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, Salim Morcane amesema
majira ya saa 9.00 usiku wa kuamkia jana Januari 24, 2025, katika eneo la
Kimalamisale, Mtaa wa Serengeti B uliopo Kata ya Dutumi, Kibaha vijijini
waliwakamata wanaume watatu na mwanamke mmoja aliyekutwa na mtoto huyo wa kike
na gari Toyota IST.
Kamanda Morcane ameeleza kuwa baada ya kumpata mtoto,
walimpeleka katika Hospitali ya Tumbi kwa uchunguzi Zaidi, kisha atakabidhiwa
kwa wazazi lakini kwa sasa yupo sehemu salama zaidi.
0 Maoni