Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza alipomwakilisha
Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye Mkutano Maalum wa Wakuu wa Nchi
na Serikali wa Umoja wa Afrika kuhusu Mpango wa Maendeleo ya Kilimo Afrika
kwenye Kituo cha Mikutano cha Speke Resort Munyonyo, Kampala Uganda, Januari
11, 2025. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitia saini mbele ya Rais Yoweri Museveni wa Uganda (kushoto) na Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika baada ya kushuhudia Tamasha la Kahawa Afrika. Africa Coffee Festival) lililolenga kuhamasisha uongezaji thahamani katika mazao yanayolimwa Afrika likiwemo zao la kahawa. Tukio hilo lilifanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Speke Resort, Munyonyo, Kampala Uganda ambako alimwakilisha Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika Mkutano Maalum wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika kuhusu Mpango wa Maendeleo ya Kilimo Afrika, Januari 11, 2025. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya
Nne Jakaya Kikwete wakiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Nchi na Serikali
wa Umoja wa Afrika baada ya Rais Yoweri Museveni wa Uganda kufungua Mkutano
Maalum wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika kuhusu Mpango wa Maendeleo ya Kilimo
Afrika kwenye Kituo cha Mikutano cha Speke Resort Munyonyo, Kampala Uganda,
Januari 11, 2025. Waziri Mkuu alimwakilisha
Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan Kwenye mkutano huo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa pamoja na baadhi ya Wakuu wa
Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika wakisikiliza wimbo wa taifa wa Uganda
katika ufunguzi wa Mkutano Maalum wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa
Afrika kuhusu Mpango wa Maendeleo ya
Kilimo Afrika uliofanyika kwenye Kituo
cha Mikutano cha Speke Resort Munyonyo,
Kampala Uganda, Januari 11, 2025. Waziri Mkuu alimwakilisha Rais Dkt Samia
Suluhu Hassan wenye mkutano huo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
0 Maoni