Moja ya matukio yaliyotia nakshi na kuacha simulizi vinywani
mwa watu siku ya leo katika Hifadhi ya Taifa Mikumi ni ile “suprize”
aliyofanyiwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na
Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa na kikundi cha “Twende na Samia 2025”.
Wanachama wa Kikundi cha “Twende na Samia 2025 - Ilala
Tumejipanga” walifika mapema ndani ya Hifadhi ya Taifa Mikumi na kum-suprize
Msigwa kwa kuja na kuungana nae kufanya “Royal Tour” kama aliyoifanya Rais
Samia.
Wanachama hao walimtaka Msigwa kuungana nao katika
kutembelea na kutangaza makubwa aliyoyafanya Rais Samia katika sekta ya Utalii
kupitia filamu ya “Royal Tour” na ile ya “Amazing Tanzania” ikiwa ni pamoja na
uwekezaji unaofanywa na Serikali katika sekta ya Utalii Nchini.
“Imekuwa siku nzuri baada ya kufanikisha safari ya Waandishi
wa Habari wa Dodoma kwa treni ya SGR hadi Morogoro ambako tuliungana na
waandishi wa Morogoro sote tumekuja Hifadhi ya Taifa ya Mikumi.
Tumeshuhudia uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali kupitia
Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) na Shirika la Reli Tanzania (TRC).
“Waandishi wote kwa wingi huu tumeweza kulala ndani ya
hifadhi malazi ni ya uhakika na ya viwango vya juu sana huku gharama ikiwa
nafuu kwa watanzania, mandhari nzuri, wanyama wengi sana huku usingizi
ukipambwa kwa sauti asilia za viumbe hai waliohifadhiwa kwa weledi na wataalamu
wetu” alisema Msigwa
Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa leo Januari 25, 2025 amefanya Mkutano na Vyombo vya Habari ndani ya Hifadhi ya Taifa Mikumi akiangazia Taarifa za Mafanikio ya Serikali hususan katika Hifadhi za Taifa.
Na. Edmund Salaho/ Mikumi
0 Maoni