CHADEMA kwa sasa imepoteza imani na mvuto - Lissu

 

Mgombea nafasi ya Uenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Tundu Lissu amesema chama hicho kimepoteza imani na mvuto kwa wafuasi wake wengi na wananchi kwa ujumla kwasababu ya uongozi wa sasa kuwa karibu na chama tawala na mamlaka kwa ujumla.

Akihojiwa na BBC Lissu, ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa sasa, amesema njia pekee ya kurudisha Imani na kutegemewa na wananchi ni kwa kupata uongozi mpya utaobadilisha mwelekeo wa chama hicho.

Chadema kinatarajia kufanya uchaguzi wa viongozi wake wa ngazi ya taifa tarehe 21 Januari, huku nafasi ya Mwenyekiti wa chama ikigombaniwa na watu wanne; Freeman Mbowe, Tundu Lissu, Odero Charles Odero na Romanus Mapunda.

Hata hivyo mchuano umekuwa mkali zaidi unatarajiwa kuwapo kati ya Lissu na Mbowe ambapo wafuasi wao, hasa katika mitandao ya kijamii, wamekuwa wakishambuliana kwa maneno na shutma mbalimbali.

Chapisha Maoni

0 Maoni