Balozi wa Marekani Michael Battle amefurahishwa na huduma
bora za usafiri wa reli ya kisasa ya (SGR) baada ya kusafiri kwa treni ya
Shirika la Reli Tanzania (TRC) kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma.
Balozi Battle ameandika katika mtandao wake wa X kuwa,
"Nimesafiri na treni katika mabara manne, na najivunia kusema kuwa
Tanzania inatoa huduma ya kipekee ya usafiri wa treni," ameandika Balozi
Battle na kuongeza,
"Treni inaondoka stesheni kwa wakati, ufafiri
ulikuwa wa utulivu, na ukarimu unaozingatia taaluma wa watumishi wake ulikuwa mzuri
sana ‘supa’."
0 Maoni