FBI imemtaja mshambuliaji wa shambulio la gari na kutumia
sialaha la New Orleans lililouwa watu 15 kuwa Shamsud-Din Jabbar mwenye umri wa
miaka 42 - mwanajeshi mkongwe na raia wa Marekani kutoka Texas.
Jabbar alikuwa amefanya kazi katika majukumu mbalimbali
katika Jeshi la Marekani, ikiwa ni pamoja na katika kitengo cha rasilimali watu
na teknolojia ya mawasiliano (IT).
Alipelekwa Afghanistan kuanzia Februari 2009 hadi Januari
2010. Jabbar alikuwa na rekodi ya uhalifu, inayohusiana na makosa ya barabarani
na wizi.
Taarifa ya FBI inasema inaamini mshukiwa wa shambulio
hilo hakutekeleza shambulio hilo peke yake.
Bendera ya ISIS ilipatikana kwenye gari la mshambuliaji huyo
aliyewaua watu 15 na kujeruhi watu wengine 35.
0 Maoni