Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Dkt. Dorothy Gwajima ametoa pole kwa wazazi wa mtoto Graison Kenyenye aliyeuawa na watu wasiojulikana, na kuwataka wazazi na walezi kuimarisha ulinzi na usalama wa watoto.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari aliyoitoa leo Desemba
27, 2024, Dk Gwajima amesema wizara yake imepokea kwa taarifa hizo za
masikitiko kwa simanzi kubwa kutokana na mtoto huyo kukatishwa uhai wakati
ndiyo kwanza alikuwa anaanza safari ya ndoto za maisha yake.
Tukio hilo limetokea Ilazo Extension jijini Dodoma
Desemba 25, 2024, wakati mfanyabiashara Zainab Shaban maarufu Jojo alipomuacha
mtoto huyo nyumbani kwa rafiki yake wa kiume ambaye ni Ofisa Uvuvi Mtera, Hamis
Mpeta.
Taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, George
Katabazi ilisema tukio hilo limetokea
Desemba 25, 2024 saa 1.00 asubuhi ambapo Mpeta akiwa na mama wa mtoto Zainab
walibaini mtoto huyo kuuawa baada ya kurejea kutoka matembezini.
Kamanda Katabazi ameeleza kuwa walimkuta mtoto huyo akiwa
ameuawa kwa kupigwa na kitu kizito kichwani na shingoni amekatwa na kitu chenje
nja kali, na kuongeza kwamba mama wa mtoto alimwacha mtoto huyo chini ya uangalizi dereva
bodaboda anayejulikana kwa jina la Kelvin Gilbert.
0 Maoni