Jaji Mwanaisha Kwariko afariki dunia India

 

Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma ametangaza kutokea kifo cha Jaji wa Mahakama ya Rufani Mhe. Mwanaisha Athumani Kwariko kilichotokea tarehe leo Desemba 27, 2024 katika Hospitali ya Max Super Speciality iliyopo nchini India alipokuwa akipatiwa matibabu. 

Taarifa fupi iliyotolewa na Mahakama ya Tanzania, imeeleza kuwa marehemu Jaji Mwanaisha Kwariko anatarajiwa kuzikwa Mkoani Dodoma, kijijini kwao Bicha Wilayani Kondoa tarehe 30 Desemba, 2024.

Chapisha Maoni

0 Maoni