Wakazi wa Manispaa ya Songea wamejitokeza kwa wingi kuvinjari
ndani ya Bustani ya Wanyamapori hai RUHILA katika siku ya kufungua zawadi za
Sikukuu ya Krismasi maarufu kwa lugha ya Kingereza kama "Boxing Day".
Jumla ya watalii wa ndani 178 waliweza kutembelea bustani
hiyo na kupata fursa ya kujionea wanyamapori mbalimbali waliopo ndani ya
bustani hiyo ikiwa ni pamoja na kufurahia muziki wa kumtoa nyoka pangoni wa Live
Band mashuhuri kutoka Manispaa hiyo.
Mbali na burudani hizo watalii, kulikuwa na nafasi mahsusi kwa watoto kucheza
michezo mbalimbali kwa kutumia vifaa vya kisasa zikiwemo "Jumping
Castle", magari ya watoto, swimming pool na mambo kadha wa kadha ya
kuondoa msongo wa mawazo kubwa zaidi ni
kujipatia Nyamapori Choma iliyoandaliwa kwa viwango vya kufunga mwaka.
Watu waote mnakaribishwa RUHILA ZOO iliyopo katikati ya
Manispaa ya Songea... “kwetu sisi furaha yako ndiyo kipaumbele chetu.”
Wasiliana naoa kwa namba +255 676 475 541 (Afisa Habari
wa TAWA) au +255 767 228 414 (Afisa Utalii wa Ruhila ZOO).
0 Maoni