Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na
Makundi Maalum Mhe Mwanaidi Ali Khamis amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan anawajali watu wenye Mahitaji Maalum
kwani ameweka mazingira mazuri ya kuwalinda na kuwapatia huduma muhimu hasa
katika Makao ya Watoto na Makazi ya Wazee yaliyopo nchini.
Naibu Waziri Mwanaidi amesema hayo jana akiwa visiwani Zanzibar
wakati akitoa zawadi za Sikukuu ya Christmas na Mwaka kwa niaba ya Rais Samia
katika Makao ya Watoto na Makazi ya Wazee Zanzibar.
"Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ni kawaida yake inapofika msimu wa Sikukuu kama
hizi kutoa zawadi Kwa watoto, wazee na wananchi ili waweze kufurahia kwa
pamoja, na leo ameona ni vema kuwafikia watu wa Zanzibar" amesema Naibu
Waziri Mwanaidi.
Aidha Naibu Waziri Mwananidi amewataka wananchi kufurahia
sikukuu za mwisho wa mwaka kwa kuwajali na wenye mahitaji Maalum ikiwa pamoja
na kuwapa msaada na mahitaji mbalimbali.
0 Maoni