Watu wawili akiwamo dereva wa bodaboda, Kelvin Joshua (27) na Tumaini Msangi (28) ambaye ni bondia, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma wakikabiliwa na kesi ya mauaji ya kukusudia ya mtoto Grayson Kanyenye (6).
Washtakiwa hao wote wakazi wa Ipagala, Jijini Dodoma,
wamefikishwa katika Mahakama hiyo leo Jumatatu, Desemba 30, 2024 mbele ya
Hakimu Mkazi, Denis Mpelembwa.
Akiwasomea mashtaka, Wakili Mwandamizi wa Serikali,
Patricia Mkina amedai wanakabiliwa na shtaka la mauaji ya Grayson Kanyenye,
yaliyotokea Desemba 25, 2024 katika mtaa wa Ilazo Kata ya Ipagala, Jijini
Dodoma.
Baada ya kusomewa mashtaka hayo, Hakimu Mpelembwa amesema
Mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza mashauri ya mauaji, hivyo hawatakiwi
kujibu chochote.
Tukio hilo lilitokea Ilazo Extension jijini Dodoma
Desemba 25, 2024, wakati mfanyabiashara Zainab Shaban maarufu Jojo alipomuacha
mtoto huyo nyumbani kwa rafiki yake wa kiume ambaye ni Ofisa Uvuvi Mtera, Hamis
Mpeta.
Taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, George
Katabazi ilisema tukio hilo limetokea
Desemba 25, 2024 saa 1.00 asubuhi ambapo Mpeta akiwa na mama wa mtoto Zainab
walibaini mtoto huyo kuuawa baada ya kurejea kutoka matembezini.
Kamanda Katabazi ameeleza kuwa walimkuta mtoto huyo akiwa
ameuawa kwa kupigwa na kitu kizito kichwani na shingoni amekatwa na kitu chenje
nja kali, na kuongeza kwamba mama wa mtoto alimwacha mtoto huyo chini ya
uangalizi dereva bodaboda anayejulikana kwa jina la Kelvin Gilbert.
0 Maoni