Aliyewahi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Mstaafu Frederick Werema amefariki dunia leo mchana tarehe 30/12/2024 katika Hospital ya Taifa Muhimbili, akiwa na umri wa miaka 69.
Taarifa za kifo chake zimetolewa na Katibu wa Parokia ya Mt.
Martha, Salome Ntaro ambayo Jaji Mstaafu Werema alikuwa Mwenyekiti wa Parokia
hiyo.
“Tujumuike na familia yake katika sala na maombolezo kwa
msiba huu mzito,” imesema taarifa hiyo ya Ntaro na kumalizia kuwa “Taratibu Nyingine
zinapangwa, tutaendelea kuwajulisha.”
Marehemu Jaji Mstaafu Werema alihuduma nafasi ya Mwanasheria
Mkuu wa Tanzania tangu mwaka 2009 hadi mwaka 2014, kabla ya hapo alikuwa Jaji
wa Mahakama Kuu Divisheni ya Biashara.
Jaji Mstaafu Werema alijiuzulu wadhifa wa Mwanasheria
Mkuu Desemba 2014, kwa tuhuma za kuridhia kuhamishwa dola milioni 120 kutoka kwenye
akaunti ya Escrow. Hata hivyo mwenyewe alisema kuwa ushauri wake haukueleweka vyema.
0 Maoni