Wanavijiji wa Kata ya Bugwema wamejawa na furaha tele baada
ya Kituo cha Afya cha kata hiyo kupokea gari jipya la wagonjwa (Ambulance) lililotolewa
na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Wanavijiji hao kutoka Kata hiyo yenye vijiji vinne
(Bugwema, Kinyang'erere, Masinono na Muhoji) wamemshukuru sana Mhe Rais Samia kwa
kuwapatia gari jipya la wagonjwa (Ambulance).
Katika hafla ya kupokea gari hilo jana iliyohudhuriwa na
Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini Prof. Sospeter Muhongo, wanavijiji hao
wamesema kuwa gari hilo kwao ni zawadi ya pekee kutoka kwa Rais, “kwetu sisi
tunaiona kama zawadi ya Krismasi.”
Wakiongea kwa nyakati tofauti wanakijiji hao wamesema
kuwa gari hilo litawasaidia mno katika kuwapeleka wagonjwa ambao wanahitaji
matibabu ambayo yameshindikana katika kituo hicho.
Kutokana na furaha waliokuwa nayo ya kutatuliwa kero ya
kukosa gari la wagonjwa wanavijiji hao wameahidi kumpatia Mhe Rais wetu kura
zote za Kata hiyo kwenye uchaguzi mkuu wa mwakani (2025).
Kwa upande wake Prof. Muhongo amemshukuru sana Mhe. Rais
Samia, na kumpongeza kwa kuendelea kuwatumikia Watanzania kwa dhati katika kuwaletea
maendeleo kwenye sekta mbalimbali zikiwamo za afya na elimu.
0 Maoni