Maneno haya
yamesema na Bi. Lilian Skawa kwa niaba ya wakinamama wa Chalinze mbele ya
Mbunge wa Jimbo la Chalinze na WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi Ajira
na Wenye Ulemavu Ndg. Ridhiwani Kikwete wakati wakipokea majiko ya gesi 118 kwa mama lishe wa kata 15
za Jimbo la Chalinze.
Ndg.
Ridhiwani Kikwete amesema lengo kubwa la kugawa majiko haya ya gesi ni kuunga
mkono juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan katika kutunza mazingira na kuwafanya
wananchi kuondokana na matumizi ya nishati chafu.
" Sasa
mtakwenda kupika chakula kwa haraka na kwa Usafi na hii itasaidia katika
shughuli zenu kwa pamoja tutamuunga Mhe. Rais Samia kwenye uhamasishaji wa
matumizi ya nishati safi ya kupikia, ambayo italinda afya zenu pia,"
amesema Ndg. Ridhiwani.
Afisa
Maendeleo ya Jamii na mratibu wa dawati la Jinsia wa Halmashauri hiyo Recho
Mnguruta amesema majiko hayo yatakwenda kuwasaidia Wanawake wajasiriamali hao
kuondokana na kutumia kuni na mkaa.
Naye Bi.
Lilian Skawa mkazi wa Msata amemshukuru Mbunge huyo wa Jimbo hilo kwa kuwapatia
majiko hayo ambayo yatawarahisishia kwenye kazi yao kupika kwa haraka na
kuwapatia wateja wao chakula cha moto muda wote.
Amesema
kipindi cha mvua walikuwa wanakabiliana na changamoto ya mkaa ambao wanapata
kwa shida na ukiwa umelowa hivyo kwasasa wanakwenda kuwa na mabadiliko ya
kupika kwa wakati chakula na kwa Hali ya Usafi.
0 Maoni