Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imeanza utekelezaji wa maandalizi ya matengenezo ya dharura ili kuzuia uvujaji wa maji katika maungio ya bomba la inchi 40 na inchi 28 katika Mtambo wa Uzalishaji Maji wa Ruvu Juu.
DAWASA
imelazimika kuzima mtambo wa Ruvu Juu kwa saa 24 ili kuruhusu matengenezo hayo
na kusababisha maeneo ya Kibaha hadi Kisarawe kukosa huduma ya maji.
Kaimu
Mkurugenzi wa Uzalishaji na Usambazaji Maji, Mhandisi Leonard Msenyere amesema
kazi inaendelea kufanyika usiku na mchana na inategemea kukamilika ndani ya
muda uliowekwa.
"Wataalam
mbalimbali tunaendelea na kazi hii usiku kucha kuhakikisha inakamilika ndani ya
muda uliopangwa na kuwezesha huduma kurejea kwa katika hali yake ya
kawaida," amesema Mhandisi Msenyere.
Mtambo wa
Ruvu Juu unahudumia maeneo ya Mlandizi, Kibaha, Ruvu Darajani, Ruvu JKT,
Visiga, Maili 35, Misugusugu, Kongowe, Soga, Miembe Saba, Kwa Mfipa,
Mwendapole, Tanita, Kwa Mathias, Kwa Mbonde, Picha ya Ndege, Lulanzi, Kiluvya,
Kibamba, Mbezi, Magari Saba, Mbezi Inn, Mbezi, Kimara,Tabata, Segerea, Kinyerezi,
Kisukuru, Bonyokwa, Msigani, Maramba Mawili, Kimara B, Kimara Korogwe, Bucha,
Baruti, Ubungo, Magomeni, Ukonga, Uwanja wa Ndege, Kiwalani, Vingunguti, Gongo
la Mboto, Pugu na Kisarawe.
0 Maoni