Bodi ya
Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) imekagua miradi ya serikali katika Wilaya ya
Kongwa na kutembelea nyumba zilizofanyiwa ukarabati mkubwa. Nyumba hizi za
gharama nafuu zimepangishwa kwa wananchi na sasa zinauzwa kupitia utaratibu wa
Mpangaji Mnunuzi.
Mradi huu ni sehemu ya juhudi za NHC kuhakikisha wakazi wa Kongwa wanapata makazi bora, salama, na yenye gharama nafuu.
Hii ni hatua kubwa katika kuboresha maisha ya
Watanzania na kuchochea maendeleo katika wilaya hii. Ziara hiyo imefanyika
baada ya kukamilisha ukaguzi wa miradi ya serikali inayotekelezwa na NHC katika
mji wa serikali Mtumba.
Kuwa sehemu
ya mafanikio haya, Furahia fursa ya kumiliki nyumba yako kupitia mpango huu wa
kipekee wa Mpangaji Mnunuzi. Tembelea NHC leo na jifunze zaidi.
0 Maoni