Ukraine yasema imemuua Luteni Jenerali Igor wa Urusi

Nchi ya Ukraine imesema imemuua Luteni Jenerali wa Urusi Igor Kirillov, ambaye amekufa kwenye tukio la mlipuko leo Jumanne Jijini Moscow.

Lt Jen. Igor Kirillov alikuwa katika eneo la kuingilia nyumbani kwake wakati bomu lililofichwa kwenye pikipiki ya umeme lilipomlipukia.

Vyanzo kutoka kwenye taasisi ya usalama wa taifa wa Ukraine, vimeliambia shirika la habari la BBC kuwa Kirillov alikuwa kwenye mpango wa kushambuliwa.

Hapo jana Jumatatu, Kirillov alifunguliwa mashtaka Jijini Kyiv kwa matumizi ya silaha za kemikali zilizopigwa marufuku.

Kirillov alishawekewa vikwazo na UK pamoja na mataifa mengine kwa uhusika wake wa Urusi kutumia silaha za kemikali.


Chapisha Maoni

0 Maoni