Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa
ametoa wito kwa Watanzania kuendelea kuishi kwa kutunza tunu za upendo, umoja,
amani na kufanya matendo ya huruma.
Bashungwa ameeleza hayo wakati alipoungana na waumini wa
Kanisa Katoliki Parokia ya Kiruruma katika Ibada ya Krismasi, leo tarehe 25
Disemba 2024.
“Tukipendana tutakuwa wamoja, tukipendana tukawa wamoja
tutakuwa na amani, lakini kuna tunu nyingine ya ujirani mwema na kufanya
matendo ya huruma,” amesema Bashungwa.
Bashungwa amesema kuwa Serikali itaendelea kushirikiana
na taasisi za kidini likowemo Kanisa Katoliki ambalo ni miongoni mwa Makanisa
yenye mchango mkubwa katika kuwakumbusha Watanzania kuishi kwa upendo na amani.
“Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Mhe. Dkt.
Samia Suluhu Hassan itaendelea kushirikia na na taasisi za dini likiwemo Kanisa
letu Katoliki kwa kuwa ni miongoni mwa makanisa yanafundisha Watanzania kuwa
raia wema,” amesisitiza Bashungwa.
Awali, Paroko Msaidizi wa Parokia ya Kiruruma, Padre
Salapioni Mberwa amewaaea Waumini wa Kanisa Katoliki kuiadhimisha Sikukuu ya
Krismasi kwa kukumbuka upendo wa Mwenyezi Mungu kwa Wanadamu.
“Mahala penye upendo kuna umoja, tunaposherekea Noeli
hii, tuenzi umoja na upendo wa Mwenyezi Mungu anaotupatia, mahali penye umoja
ndipo penye amani,” amesema Padre Salapioni.
0 Maoni