Makumi ya watu wamenusurika kifo katika ajali ya ndege
iliyoanguka ikiwa na abiria 67 huko
Kazakhstan.
Maafisa wa nchi hiyo wamesema jumla ya watu 38 wamekufa
katika ajali hiyo.
Ndge hiyo ya shirika la ndege la Azerbaijan namba J2-8243
iliwaka moto wakati ikitua kwa dharura karibu na mji wa Aktau nchini
Kazakhstan.
Ndege hiyo iliyokuwa ikielekea nchini Urusi, ililazimika
kubadili safari yake kutokana na hali ya hewa ya ukungu.
Picha zilionyesha ndege hiyo ikiwa inatua kwa kasi kali
huku matairi yakiwa chini na ghafla ikalipuka moto ikitua.
0 Maoni