Jamii imehimizwa kuwakumbuka watu wenye Mahitaji Maalum
katika msimu huu wa Sikukuu kwa kuwapatia zawadi na mahitaji mbalimbali ili
waweze kusheherekea kwa furaha sikukuu za mwisho wa mwaka.
Rai hiyo imetolewa jana na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake Jinsia na Wanawake na Makundi Maalum,
(anayeshughulikia Maendeleo ya Jamii na Makundi Maalum) Wakili Amon Mpanju
wakati akikabidhi zawadi mbalimbali kwa watoto wanaolelewa katika Makao ya ya
Taifa ya Watoto Kurasini Dar es Salaam, kwa niaba ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu
Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
"Msimu wa Sikukuu jamii inapaswa kuwakumbuka na
kuwasaidia watu wenye mahitaji Maalum kama wezee na watoto wanaoishi katika
mazingira hatarishi ni jambo la baraka na linatoa matumani Kwaao na kujiona ni
kama watu wengine," amesema Wakili Mpanju.
Aidha, Wakili Mpanju ametoa wito kwa Mashirika, Taasisi
za Serikali, Mashirika yasiyo ya Kiserikali na jamii kuhakikisha watoto, wazee
na watu wenye mahitaji Maalum wanasherehekea kwa furaha Sikukuu za mwisho wa
mwaka kwa kuwakumbuka kwa zawadi na mahitaji mbalimbali ya kibinadam.
Kwa upande wake Makamu Mfawidhi wa Makao hayo Farida
Ismael amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa zawadi hizo ambazo zitawasaidia
watoto kula na kunywa na kufurahia sikukuu za mwisho mwaka kama watoto wengine.
Naye mmoja wa mtoto anayelelewa katika Makao hayo Festo
Elias kwa niaba ya watoto wenzake amemshukuru Rais Samia kwa kuwakumbuka watoto
katika kipindi hiki cha Sikukuu na ameeleza kufurahia zawadi hizo na kuomba
wadau na taasisi zingine kufanya hivyo mara kwa mara.
0 Maoni