Shirika la Reli Tanzania (TRC) limesema kuwa mabehewa 264
ya mizigo yatakayotumika katika reli ya kiwango cha kimataifa (SGR) yamewasili katika
Bandari ya Dar es Salaam jana Desemba 24, 2024 yakitokea nchini China.
Taarifa ya TRC iliyotolewa leo imesema kwamba baada ya
kukamilika kwa zoezi la kuyashusha mabehewa hayo kutoka kwenye meli, litafuata
zoezi la majaribio kwa kutembeza mabehewa hayo yakiwa matupu na kisha yakiwa na
mizigo.
Taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano wa TRC,
Fredy Mwanjala imesema kwamba mabehewa hayo ya mizigo, treni yake itakuwa
inatembea kwa kasi ya kilometa 120 kwa saa.
0 Maoni