TRC yaongeza safari za treni mikoa ya kaskazini

 

Shirika la Reli Tanzania (TRC) limeongeza safari za treni kuelekea sikukuu za mwisho wa mwaka kwa safari za kuelekea mikoa ya Tanga, Kilimanjaro na Arusha na kusema kuwa hakutakuwa na ongezeko la nauli.

Taarifa ya Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano TRC Fredy Mwanjala imesema kuwa siku ya Jumatano itaongezeka kujumuisha siku za Jumatatu na Ijumaa hivyo kufanya jumla ya safari tatu kwa juma kuelekea mikoa hiyo.

Pia, kila siku ya Jumatano ya juma Desemba 09, mwaka huu mpaka mwanzoni mwa Januari 2025, TRC itapeleka mabehewa 18 yatakayobeba abiria zaidi ya 1,000 kwa wakati mmoja kulekea katika mikoa hiyo.

Katika taarifa yake hiyo TRC imesema ongezeko hilo ni hatua mahususi ya kukabiliana na ongezeko la abiria katika kipindi hiki hususan kuelekea mikoa ya Kaskazini Mashariki mwa Tanzania.



Chapisha Maoni

0 Maoni