Safari ya
mabalozi kupanda Mlima Kilimanjaro, hatimaye imesalia muda wa saa 96 kukifikia kilele kirefu zaidi barani Afrika cha Uhuru chenye urefu wa mita 5895 kutoka
usawa wa bahari.
Safari ya
siku sita ya kuelekea kilele cha Uhuru ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 63
ya Uhuru wa Tanganyika imeingia siku ya pili baada ya mabalozi wanaoiwakilisha
Tanzania nchi za nje kuendelea kupunguza vituo 2 na kubakiwa na vituo 3 kati ya
vituo 5 hadi kileleni.
Safari ya
kuukwea mlima huo huchukua takribani saa 144 ikiwa ni sawa na siku 6, lakini
hadi jana jioni, waheshimiwa mabalozi hao walikuwa wamebakiza saa 96 kukifikia
kilele hicho.
Mabalozi
walioanza safari ya kuelekea katika kilele hicho kirefu kuliko vyote barani
Afrika kupitia lango la Marangu ni pamoja na Mhe. Balozi Gelasius Byakanwa (Burundi),
Mhe. Balozi Prof. Adelardus Kilangi (Brasilia) na Mhe. Balozi (IGP Mstaafu)
Simon Sirro (Zimbabwe).
Wengine ni Mhe.
Balozi Saidi H. Massoro (Kuwait), Mhe. Balozi Innocent Shiyo (Ethiopia), Mhe.
Balozi Dkt. Mahadhi J. Maalim (Malaysia), Mhe. Balozi Habibu A. Mohamed (Qatar), Mhe. Balozi Baraka Luvanda (Japan) na Mhe. Balozi Mej. Jen. Richard M.
Makanzo (Misri).
0 Maoni