Jamshid bin Abdullah, Sultani wa mwisho kuitawala
Zanzibar na aliyeondolewa mamlakani kwa mapinduzi ya Januari 1964 amefariki
dunia.
Jamshid amefariki hospitalini nchini Oman jioni ya jana
Jumatatu, Desemba 30 akiwa na umri wa miaka 95.
Sababu za kifo chake zinaelezwa kuwa ni maradhi ya muda
mrefu na uzee. Anatarajiwa kuzikwa leo Jumanne katika makaburi ya kifalme
jijini Muscat, Oman.
0 Maoni