Angelina Jolie na Pitt waafikiana makubaliano ya talaka

 

Nyota wa filamu wa Hollywood Angelina Jolie na Brad Pitt wamefikia maafikiano ya makubaliano ya talaka, baada ya miaka minane ya kuchuana kisheria.

Wanandoa hao walifunga ndoa 2014, wanawatoto sita, ni mingoni mwa nyota wakubwa katika sekta ya burudani na walipachikwa jina la 'Brangelina' na vyombo vya habari.

Jolie alifungua madai ya talaka mwaka 2016, akitaja sababu za “kuwapo kwa tofauti zisizoweza kupatanishwa.”

Hata hivyo, baadae ilikuja kubainika kuwa Pitt anatuhumiwa kwa kumnyanyasa mkewe pamoja na watoto wao wawili wakiwa kwenye ndege mwaka huo.

Hata hivyo Pitt hakufunguliwa mashtaka baada ya polisi kuchunguza tukio hilo na amekanusha tuhuma hizo.

Chapisha Maoni

0 Maoni