Sita wafaka kwenye ajali Mbinga wakiwamo walimu wanne

 

Watu sita wamepoteza maisha katika ajali ya gari aina ya Prado lenya namba T 647 CVR, iliyokuwa inatokea mpakani mwa wilaya za Mbinga na Nyasa kwenye eneo la Chunya leo Desemba 28, 2024.

Ajali hiyo imesababisha vifo vya walimu wanne wa Shule ya Msingi Lumaru, Mfamasia mmoja na dereva wa gari hilo waliokuwa wakienda katika Shule ya Sekondari Limbo iliyopo wilayani Nyasa.

Akizungumzia ajali hiyo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Marco Chilya amesema ajali hiyo imetokea katika Kijiji cha Lumalu Kata ya Upolo leo saa 1:10 asubuhi, ambapo gari hilo gari lililogonga gema na kuwaka moto katika Kijiji cha Lumala.

Kamanda Chilya ameeleza kwamba chanzo cha ajali ni uzembe wa dereva wa gari hilo  kushindwa kuchukua tahadhari kutokana na kona nyingi na mteremko katika Wilayani Mbinga.

Chapisha Maoni

0 Maoni