Hospitali ya Taifa Muhimbili Mloganzila imemkamata Bw.
Steven K. Julius kwa tuhuma za wizi wa mali za wa wagonjwa ikiwemo simu za
wagonjwa waliolazwa hospitalini hapo kwa kujifanya ni mwajiriwa wa Muhimbili
Mloganzila kwa cheo cha Afisa Muuguzi.
Baada ya mahojiano Bw. Julius amekiri kuiba simu tatu
ambapo mbili aliziuza kwa mkazi wa Kibamba na moja ameiuza kwa mtu anyeishi nje
ya mkoa wa Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Bw. Julius baada ya kumaliza mafunzo kwa
vitendo ya uuguzi (nursing internship) amefanya kazi katika hospitali kadhaa za
mkoa wa Dar es Salaam ambapo alifukuzwa kutokana na vitendo vya kukiuka maadili
ikiwemo wizi.
Mtuhumiwa amefikishwa Kituo cha Polisi Gogoni kilichopo
Kibamba kwa taratibu za kisheria.
Aidha, uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili unapenda
kuihakikishia jamii kuwa inayo mifumo imara ya kiusalama ya kuweza kubaini watu
wote wanaoingia na kutoka hospitalini na ndio maana imeweza kumfuatilia
mtuhumiwa huyu na kumkamata.
0 Maoni