Watu wapatao 151 wamekufa baada ya ndege kuanguka wakati
ikitua kwenye uwanja wa ndege Korea Kusini.
Ndege hiyo aina ya Boeing 737-800 ya shirika la Jeju Air,
ilikuwa na abiria 181 ikiwasili kwenye uwanja wa ndege wa Muan ikitokea Bangkok
nchini Thailand.
Picha za mitandao ya jamii zinaionyesha ndege hiyo ikitoka
nje ya njia ya kutulia na kujibamiza kwenye ukuta, kisha kulipuka moto.
Bado hakijajulikana chanzo cha ajali hiyo, lakini vikosi
vya zimamoto vinaamini iligongana ndege ama ni kutokana na hali mbaya ya hewa.
0 Maoni