Mgombea wa
upinzani na Rais wa zamani wa Ghana John Dramani Mahama ametangazwa rasmi kuwa
mshindi katika uchaguzi wa urais Ghana uliofanyika mwishoni mwa juma.
Mahama alijipatia
ushindi wa asilimia 56.6 za kura zote zilizopigwa huku mpinzani wake makamu wa
Rais wa sasa Mahamudu Bawumia akiambulia asilimia 41.6 ya kura.
Ni ushindi
mkubwa zaidi katika nchi hiyo kwa miaka 24. Waliojitokeza kupiga kura walikuwa
ni asilimia 60.9, alisema Mkuu wa Tume ya Uchaguzi nchini Ghana, Jean Mensa.
Mahama amesema
anahisi “kufurahishwa” na kwamba yeye na chama chake cha National Democratic
Congress (NDC). “Wamepiga kura moja ya matokeo mazuri katika historia ya
uchaguzi wa Ghana.”
Mahama
aliahidi kuleta “mwanzo mpya, mwelekeo mpya” na akabainisha kuwa Ghana imeweka
historia kwa kumchagua makamu wa rais wa kwanza mwanamke Jane Naana Opoku
Agyemang.
0 Maoni