Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amemtaka Mkurugenzi
Mtandaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Prof. Mohamed Janabi kujiandaa
kugombea nafasi ya aliyekuwa Mkurugenzi wa Shirika la Shirika la Afya Duniani
(WHO) Kanda ya Afrika, Dkt. Faustine Ndugulile.
Dkt. Janabi
ambaye ameteuliwa na Rais hivi karibuni kuwa Mshauri wa Rais Masuala ya Afya na
Tiba, ameambiwa kujianda kwa nafasi hiyo ya Dkt. Ndugulile ambaye pia alikuwa
Mbunge wa Kigamboni, aliyefariki dunia Novemba 27, 2024 ikiwa ni miezi kadhaa kupita
tangu ashinde nafasi hiyo.
Akizungumza
mara baada ya kuwaapisha viongozi mbalimbali leo Desemba 10, 2024 kwenye Ikulu
Ndogo ya Tunguu, Zanzibar, Rais Samia amesema wamepitia wasifu nyingi na
kubaini kwamba, Profesa Janabi ana sifa ya kurithi mikoba ya marehemu Dkt.
Ndugulile.
“Naomba
nifichue siri hapa, tumepitia CV kama tano na tukaona Prof. Janabi anafaa
kuchukua nafasi ya Dkt. Ndugulile, Hivyo, tunakundaa kwenda kugombea nafasi
hiyo muda utakapofikia. Ujiandae,” amesema Rais Samia.
0 Maoni